Waimbaji wa kwaya kuu kibangu wakiwa kwenye Uzinduzi! Wa kwanza ni Mr Robert Msuya, Mrs Moshi, Mr Mariki, Mama Mgeni, Mrs Masue, Lucy Malya, Jonasi Mkanza na Katibu Stephen Muwanga.
Mfalme mkuu yuko juu, Mfalme mkuu yuko juu! Ndivyo wa wanavyoimba waimbaji hawa wa kwaya kuu kibangu siku ya uzinduzi wa Toleo la Pili 2008. Wakiongozwa na Mwenyekiti Msaafu Rehema Sanga kushoto na kulia ni Twelusigwe Mwaisango. Mlezi wa kwaya Bwana Laizer aliyevaa shati la kitenge Akifuhahia
Uimbaji ni mahubiri, pia uimbaji huleta afya hasa wenye matatizo ya msongo wa mawazo, hufundisha tena huelimisha sana! Picha ni kwaya kuu Kibangu wakiimba kwenye Ibada. Mwalimu Erasto Lihawa akiimbisha.
Katika maandalizi ya mwisho mwisho kuelekea kwenye uimbaji wa Reformation 2010. Mwalimu E. Silayo akitoa maelekezo ya mwisho mwisho Mara baada ya kuonyesha uimbaji kwenye ibada na kugundua kasoro hapo alikuwa anarekebisha Baadhi ya sauti.Aliyeshika Mfuko ni Emaculata Mkichwe, na mama Kihanga. Nyuma ni Stephen Muwanga pamoja na Fadhil .
Mchungaji kiongozi Usharika wa Kibangu Richard Hananja akiwa na mgeni rasmi siku ya uzinduzi wa albam ya pili ya kwaya ya TULIA UTAFAKARI Vol. 2 . pembeni ni mwenyekiti na katibu wa kwaya.
Waimbaji wa kwaya kuu kibangu siku ya uzinduzi wa albam yao, kuanzia kulia ni Rehema Sanga, Twelusigwe Mwaisango, Frida Kihanga, Glads Musunga, Eliza Nganyule, Monica Mbwambo, Eliudika Shoo na Robert Msuya.